Mteja…

Mteja mbona hupatikani? 
Sikuoni mtaani, nakukosa hadharani
Hupiti tena njiani?
Mteja mbona hupatikani? 
Nakutamani sana jamani…

Nimeuliza tena jirani
Suleimani na duka lake fulani
Mwisho kusikika sokoni 
Mteja mbona hupatikani? 
Pengine Ijumaa? Usichelewe jamaa…

Mashariki Afrika kusini
Magharibi mwa kaskazini 
Nimerudi tena mpakani
Mteja mbona hupatikani?
Mengi masaa, Nasumbuka jamaa…

Nakaa hapa sebuleni
Biriani, majani, televisheni
Sipati tena afueni
Mteja mbona hupatikani?
Nakata tamaa, Nafadhaika jamaa…

Nimechoka kupiga foleni
Kutafuta yako anwani
Nasikitika ndani moyoni
Mteja mbona hupatikani? 
Naona balaa, Silali jamaa…

Naelekea tena kanisani
Sala kuitia maanani
Kwani Mungu sio Athumani
Mteja mbona hupatikani?
Nakutamani sana jamani!

_________

Tesha Mongi © 2010

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s